MAPISHI: Drop scones

MAPISHI: Drop scones

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • Vikombe 4 unga wa ngano (self-raising)
  • Vijiko 2 vya sukari
  • Kijiko 1 cha chumvi
  • Kikombe 1 maziwa
  • Mayai 2
  • Kikombe ½ siagi iliyoyeyushwa
  • Kijiko 1 cha vanilla

Maelekezo

Kwenye bakuli, changanya vizuri unga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi.

Unga wa ngano kwenye bakuli safi. Picha/ Margaret Maina

Kwenye bakuli jingine, koroga mayai, maziwa, vanilla na siagi mpaka vichanganyike vizuri.

Mwagia mchanganyiko kwenye bakuli la mchanganyiko wa unga. Koroga.

Weka kikaangio mekoni kwenye moto wa wastani.

Mwagia robo kikombe ya unga kwenye kikaangio kilichopata moto na kupakwa siagi au mafuta ya kupikia kiasi.

Drop scones katika hatua ya mwanzo kabisa. Picha/ Margaret Maina

Pika mpaka upande wa chini uwe kahawia.

Drop scones. Picha/ Margaret Maina

Geuza upande wa pili kisha upake siagi upande wa juu ulioiva. Geuza paka siagi upande wa chini. Rudia kwa unga uliobakia mpaka umalize zote.

Pakua na ufurahie.

You can share this post!

Wakenya wapuuza kilio cha magavana

Ni mwenye nguvu nipishe The Eagles wakiwania 3-bora

adminleo