MAPISHI: Fish cakes

MAPISHI: Fish cakes

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 30

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • fish fillet (steki ya samaki isiyokuwa na mifupa) kipande kikubwa
 • viazi 6 vya wastani
 • kitunguu kikubwa
 • tangawizi na saumu kijiko 1
 • chenga za mkate – breadcrumbs – kiasi
 • mayai 2
 • limau 1
 • chumvi kiasi
 • pilipili
 • curry powder kijiko ½
 • mafuta ya kukaangia
 • majani ya giligilani

Maelekezo

Chemsha viazi na chumvi kidogo kisha viponde na uviweke pembeni vipoe.

Katakata samaki vipande kisha tia kwenye sufuria pamoja na tangawizi, kitunguu saumu, limau na chumvi.

Chemshe kiasi na uhakikishe maji yote yanakauka kisha ponda na uma.

Baada ya hapo, tia viungo vyote, pilipili na vitunguu vilivyokatwa vikawa vipande vidogovidogo na upike pamoja na samaki kwa muda wa dakika tatu.

Baada ya hapo, tia majani ya giligilani na kamulia limau kisha weka pembeni.

Sasa changanya viazi pamoja na mchanganyiko wa samaki kisha tengeneza maduara ya wastani.

Piga mayai katika bakuli na uweke chumvi kidogo.

Bandika mekoni kikaangio halafu mimina mafuta ya kukaangia; yawe kidogo tu (shallow fry). Yakishapata moto kiasi, chukua madonge yako kisha yachovye katika mayai na umalizie katika breadcrumbs kisha kaanga kwenye mafuta.

Baada ya muda kiasi, chakula chako kitakuwa tayari.

Pakua na ufurahie.

 • Tags

You can share this post!

Nitawapa mashine za kisasa kuchapa kazi nikiingia Ikulu...

Maafisa sita wa polisi waliohusishwa na mauaji ya ndugu...