Makala

MAPISHI: Jinsi ya kuandaa mbuzi ulaya

January 17th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

Muda wa kuandaa: Dakika 30

Muda wa kupika: Dakika 50

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • 1½ kilo nyama ya mbuzi ulaya
  • kijiko 1 cha chumvi
  • kijiko 1 cha pilipili manga
  • kijiko 1 cha kitunguu saumu cha unga
  • kijiko 1 cha paprika
  • kijiko 1 cha oregano
  • kijiko 1 cha udaha; yaani cayenne pepper
  • 250g ya BBQ sauce

Maelekezo

Paka nyama chumvi, pilipili manga, kitunguu saumu, paprika, cayenne pepper na oregano.

Paka vizuri kwa mkono viungo kisha paka nusu ya BBQ sauce pande zoze zishike vizuri.

Weka nyama kwenye slow cooker.

Pika kwa muda wa saa 3 au mpaka zilainike kama utakavyopenda.

Hamishia nyama kwenye chombo cha kuokea kwenye ovena.

Weka aluminium foil kwa ajili ya majimaji yatakayomwagika.

Paka BBQ sauce iliyobakia pande zote za nyama.

Oka kwa moto wa juu kwa dakika 8

Pakua na ufurahie pamoja na chipsi, viazi vya kuponda au chochote ukipendacho.