Makala

MAPISHI: Jinsi ya kuoka keki aina ya Red velvet

August 6th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 30

Muda wa kupika: Dakika 40

Walaji: 6

Vinavyohitajika

 • kikombe ½ siagi
 • kikombe 1 ½ ya sukari nyeupe
 • mayai 2
 • vijiko 2 vya cocoa powder
 • kijiko ¾ cha rangi nyekundu ya chakula (red food colour)
 • kijiko 1 cha chumvi
 • kijiko 1 cha vanilla extract
 • kikombe 1 buttermilk
 • vikombe 4 unga wa ngano
 • kijiko 1½ cha baking soda
 • siki (vinegar) vijiko 4

Maelekezo

Washa ovena joto la nyuzi 175.

Paka siagi kwenye vyombo viwili vya kuokea. Weka siagi na sukari kwenye bakuli kubwa; piga mpaka ilainike vizuri.

Ongeza yai moja moja, endelea kupiga mpaka ilainike vizuri kabisa.

Kwenye bakuli nyingine, changanya buttermilk, cocoa powder, chumvi, rangi ya chakula na vanilla extract.

Ongeza mchanganyiko wa buttermilk na unga wa ngano kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa awali (siagi, sukari na mayai), mpaka vyote vichanganyike kabisa.

Kwenye bakuli ndogo au bilauri, changanya siki na baking soda. Ongeza kwenye mchanganyiko wa keki. Changanya vizuri kutumia kijiko ila usichanganye sana.

Mwagilia mchanganyiko kwenye vyombo vya kuokea. Oka kwa nusu saa au iive vizuri. Ikiiva, epua kisha acha ipoe.

Paka icing sugar halafu katakata na ufurahie.