Makala

MAPISHI: Jinsi ya kupika mboga mchanganyiko

June 27th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa kupika: Dakika 15

Walaji: 2

MBOGA za majani zina faida nyingi za kiafya, hii ikiwa ni kutokana na ukweli kwamba:

Zina vitamini kwa wingi.

Zina madini kwa wingi.

Baadhi ni kama Dawa za kulinda afya.

Mboga za majani zinasaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Mboga za majani pia husadia kupunguza, kurekebisha na kuweka uzito sawa.

Mboga mchanganyiko. Picha/ Margaret Maina

Vinavyohitajika

  • Pilipili mboga 3 za rangi tofauti
  • Bamia
  • Karoti
  • Vitunguu maji
  • Mafuta ya kupikia
  • Chumvi

Maelekezo

Kata kitunguu. Weka kwenye chombo pembeni.

Kata karoti, osha bamia, kata na kisha weka kando.

Weka sufuria au kikaangio jikoni. Ongeza mafuta na acha yapate moto.

Weka kitunguu, koroga kiasi. Ongeza bamia, koroga zaidi. Kisha funika kwa muda ili vipate kuiva kwa muda.

Weka pilipili mboga, koroga ili vipate kuchanganyika. Ongeza karoti na uchanganye.

Ongeza chumvi na kisha koroga vizuri ili ipate kuenea vizuri.

Funika mchanganyiko kwa muda wa dakika 10.

Acha ichemke vizuri huku ukigeuza kidogo na kisha funika tena kwa dakika tano.

Pakua na chakula unachopenda.