Makala

MAPISHI: Jinsi ya kupika omena kwa kutia nazi

November 5th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Omena mbichi. Picha/ Margaret Maina

Vinavyohitajika

  • dagaa kilo ½
  • pilipili mboga 2
  • curry powder vijiko 2
  • limau 1
  • chumvi
  • pilipili kama unapenda
  • kitunguu saumu punje 3; menya na saga
  • nyanya 3
  • tomato paste

Maelekezo

Toa uchafu kwenye dagaa. Unaweza kukata vichwa ukipenda. Osha kwa makini.

Andaa kitunguu maji kwa kumenya kisha kata vipande vidogovidogo. Kata pilipili mboga vipande vidogo.

Weka kikaangio mekoni, mimina mafuta ya kupikia kiasi kisha weka kitunguu saumu huku ukikoroga.

Weka kitunguu maji kiive hadi kiwe na rangi ya kahawia. Ongeza chumvi na dagaa kwenye sufuria. Koroga vizuri kisha funika na acha dagaa wakaangike kiasi kwenye mafuta.

Ongeza nyanya, koroga pamoja vichanganyike kisha funika halafu acha viendelee kuiva vizuri bila kukauka sana.

Baada ya dakika 10, ongeza pilipili mboga na pilipili za nyembamba za kijani. Koroga vizuri kisha funika.

Sosi ya nyanya ikishaiva, weka curry powder. Koroga pamoja vizuri. Kamulia juisi ya limau huku ukikoroga vizuri. Acha ichemke kwa muda wa dakika tano.

Pakua na ufurahie kwa sima.