Makala

MAPISHI na UOKAJI: Keki aina ya Black Forest

May 7th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Keki aina ya Black Forest. Picha/ Margaret Maina

 

Muda wa kuanda: Dakika 30

Mapishi: Dakika 50

Walaji: 5

Vinavyohitajika

 • unga wa ngano kilo ½
 • cocoa powder vijiko 3
 • baking soda kijiko kimoja na nusu
 • chumvi kijiko kidogo
 • sukari nyeupe gramu 350
 • mayai 2
 • kijiko 1 cha vanilla essence
 • maziwa kikombe 1
 • siagi
 • castor sugar
 • maple syrup
 • kijiko 1 kidogo cha kahawa ya unga
 • matunda ya cherry au strawbery
 • heavy whipping cream
 • chocolate block

Maelekezo

Washa ovena iwe na joto kiasi cha nyuzijoto 175 Degrees Celsius.

Weka karatasi aina ya grease proof kwenye chombo chako cha mviringo cha kuokea. Hii itasaidia keki isiungue.

Kisha unafaa kuchanganya unga wa ngano, cocoa, baking soda na chumvi kiasi cha kijiko kidogo cha chai.

Chukua lita moja ya heavy cream uchanganye na sukari nyeupe. Koroga hadi krimu iwe nyepesi kama povu kabla ya kuongeza mayai na vanilla.

Mimina unga wa ngano uliokuwa umeuchanganya na kakau taratibu kwenye ule mchanganyiko wa sukari na cream ukichanganya kwa kutumia mkono. Mchanganyiko wako utakuwa mzito na ndiposa unafaa kumimina maziwa huku ukichanganya kwa kutumia mwiko mpaka vichanganyike vizuri. Sasa mimina kwenye vyombo vyako viwili vya kuokea keki hiyo.

Oka kwa dakika 40 na ikishaiva epua na uache keki yako ipoe kabla ya kuibandua ile karatasi.

Kata keki yako nusu ili iwe mduara dufu kisha nyunyizia maple syrup kwenye keki yako katika sehemu ya kati na juu vilevile.

Kwenye bakuli, koroga siagi mpaka iwe laini. Ongezea caster sugar, chumvi, na kahawa.

Ipake mchanganyiko huu pamoja na matunda ya cherries.

Katika bakuli tofauti kabisa koroga cream kisha uipake juu ya keki.

Mwagilia juu curls za chokoleti ulizokwangua kutoka kwenye chocolate block.

Furahia keki yako kwa juisi au kinywaji ukipendacho.