Makala

MAPISHI: Keki ya karoti

May 18th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KUANDAA: Dakika 20

Mapishi: Dakika 60

Walaji : 4

Vinavyohitajika

 • Mayai manne
 • Siagi kiasi cha kikombe kimoja na robo
 • Sukari nyeupe vikombe viwili
 • Vanilla kiasi cha vijiko viwili vya chai
 • Unga vikombe viwili
 • Baking powder vijiko viwili vya chai
 • Chumvi kiasi cha kijiko cha chai
 • Mdalasini vijiko viwili vya chai
 • Karoti gramu 250
 • Baking soda kijiko kimoja
 • Poda ya Nutmeg kiasi cha nusu kijiko cha chai
 • Buttermilk kiasi cha robo tatu za kikombe cha kawaida
 • Flaked coconut kikombe kimoja

Maelekezo

Washa ovena weka nyuzi joto 350° F

Chukua bakuli weka unga, sukari, baking powder, baking soda, mdalasini, nutmeg, na chumvi kisha changanya vizuri. Weka pembeni.

Chukua bakuli ingine weka mayai, siagi, vanilla na flaked coconut halafu koroga mpaka viwe laini kabisa.

Mchanganyiko wenye mayai mwagia kwenye unga kisha koroga mpaka uone vimechanganyikana vizuri.

Chukua karoti ulizoziandaa ukazikwangua uzitie kwenye mchanganyiko ule wa keki. Koroga vizuri sana.

Chukua chombo unachotumia kuokea keki yako ukipake siagi.

Chukua mchanganyiko wa keki mwagia kwenye chombo hicho kisha weka kwenye ovena.

Dakika 45 zikipita, funua angalia kama keki imeiva. Chukua kisu ukidungie katikati ya keki, kikitoka kikavu basi keki itakuwa imeiva. Ikiwa bado, irudishe kwenye ovena ili iive jinsi inavyotakikana.

Baada ya muda mchache chakula chako kitakuwa tayari kuliwa.