NA MARGARET MAINA
WATU wengi hufurahia kula sandiwichi kama kiamsha kinywa lakini pia ni chakula cha kuliwa wakati wowote.
Ni rahisi kutengeneza na kula pia.
Muda wa kuandaa: Dakika 5
Muda wa mapishi: Dakika 10
Walaji: 2
Vinavyohitajika
Maelekezo
Koroga mayai, maziwa na chumvi kiasi.
Weka kikaangio kwenye jiko kisha mimina mafuta kwenye kikaangio.
Mafuta yakishapata moto weka mchanganyiko wa mayai yako na kaanga yaive, ongeza jibini kisha geuza upande wa pili nao uive vyema.
Chukua kipande cha mkate na upake karanga ya siagi na kipande kingine paka Blueband.
Weka yai lako katikati ya vipande vya mkate, kata kipembezoni na sandiwichi yako ipo tayari kuliwa.
Sandiwichi hii yaweza kuliwa na kinywaji chochote chaguo lako.