MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa kari ya nyama ya ng’ombe

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa kari ya nyama ya ng’ombe

NA MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

KWA kutengeneza mlo huu, unaweza kutumia vitunguu vingi vyekundu, nyanya, pilipili, na majani ya gilgilani katika mapishi.

Kari hii ya nyama ya ng’ombe inaweza kuliwa kwa wali, viazi, au ugali.

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda w a mapishi: Dakika 40

Walaji: 2

Vinavyohitajika

 • vikombe 4 vya maji
 • nyama ya ng’ombe kilo 1
 • punje 5 za kitunguu saumu; saga
 • vijiko 2 vya tangawizi iliyosagwa
 • vijiko 2 vya mafuta ya kupikia
 • vitunguu maji 2 vyekundu, vilivyokatwa vizuri
 • nyanya 4 zilizokatwa
 • vijiko 2 vya paprika
 • kijiko ½ cha pilipili nyeusi
 • vijiko 2 vya poda ya kari
 • vijiko 4 vya nyanya ya kopo
 • chumvi kwa ladha
 • pilipili kama vile jalapeno iliyokatwa kwa ajili ya kupamba
 • majani ya giligilani

Maelekezo

Chemsha vikombe vinne vya maji katika sufuria kwenye moto wa juu. Ongeza nyama ya ng’ombe, vitunguu, na tangawizi, kisha ukoroge vizuri.

Punguza moto uwe wa wastani, funika na uwache vichemke, ukikoroga mara kwa mara kwa dakika 20.

Ondoa kutoka kwenye moto, na kwenye supu, lakini hifadhi supu hiyo kwa ajili ya matumizi katika hatua za baadaye.

Rudisha sufuria kwenye moto wa kati na vijiko viwili vya mafuta ya kupikia. Mara tu mafuta yanapokuwa moto, ongeza vitunguu na kaanga, huku ukichochea mara kwa mara, hadi kulainika, kutoka dakika tano hadi dakika saba.

Ongeza nyanya kwa vitunguu, na uendelee kupika, ukichochea mara kwa mara, mpaka nyanya zipunguke, dakika tatu hadi tano.

Ongeza nyama iliyokatwa kwenye mchanganyiko wa nyanya na vitunguu, na uchanganye vizuri. Endelea kupika juu ya moto wa kiwango cha kadri kwa dakika tano huku ukichochea mara kwa mara.

Ongeza paprika, pilipili, poda ya kari, nyanya ya kopo, na chumvi, na koroga vizuri.

Ongeza ile supu kutokana na mapishi ya nyama ya ng’ombe, pamoja na maji ya ziada ya kufunika. Chemsha kwa moto wa wastani, bila kufunika kwa muda wa saa moja, au mpaka nyama iwe laini na mchuzi uwe mzito.

Ongeza maji ya ziada ikiwa kari yako ya nyama itaanza kukauka na kushikamana, au ikiwa ungependa kari yako iwe na uthabiti zaidi wa supu.

Wakati kari ya nyama iko tayari, toa kutoka kwa moto, ionje, na urekebishe viungo unavyotaka. Pamba na pilipili na majani ya giligilani.

Pakua na ufurahie.

 • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Pasta ya kuku yenye krimu na uyoga

MAPISHI KIKWETU: Pancakes za shayiri, ndizi na iliki

T L