Na MARGARET MAINA
Muda wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa mapishi: Dakika 0
Walaji: 3
Vinavyohitajika
Maelekezo
Menya tangawizi na vitunguu saumu kisha vitwange.
Katakata nyama yako vizuri kisha ioshe.
Weka nyama kwenye bakuli kubwa au sufuria kisha mimina mafuta ya kupikia. Kisha weka tangawizi, kitunguu saumu, pilipili manga, unga wa pilipili nyekundu (red pepper), mtindi, hiliki, na mdalasini. Baada ya hapo, changanya na uache mchanganyiko huo kwa muda wa saa nne ili nyama ilainike.
Muda huo ukishaisha, washa moto na uweke sufuria mekoni. (Hakikisha moto ni mkali kiasi)
Weka mafuta kiasi kwenye sufuria.
Weka kitunguu maji kisha koroga hadi kiwe kahawia.
Weka mchanganyiko wa nyama na viungo vingine.
Funika.
Acha nyama ichemke kwa dakika 15 kisha koroga.
Funika na usubiri kwa muda wa dakika 10 hivi.
Punguza moto kidogo na acha kwa dakika 15 nyingine.
Angalia kama nyama imelainika. Ikiwa iko tayari, basi ni wakati mwafaka wa kuiepua.
Pakua na ufurahie kwa ama wali, chapati, ugali au chochote ukipendacho.