MAPISHI KIKWETU: Kaimati za mboga

MAPISHI KIKWETU: Kaimati za mboga

NA PAULINE ONGAJI

  • Viungo unavyohitaji
  • Unga wa ngano, kilo – ½
  • Maji au maziwa, lita – ½
  • Sukari, gramu – 200
  • Siagi, vijiko vya meza – 2
  • Chachu vijiko vya chai – 1
  • Mafuta ya kukaanga, kilo – ½
  • Karoti zilizokunwa, kikombe – ¼
  • Kitunguu saumu, kijiko cha chai – ½

Jinsi ya kutayarisha

Changanya unga wa ngano, chachu na sukari, kisha uchunge mchanganyiko.

Kwenye bakuli tofauti, changanya maziwa yaliyopashwa moto pamoja na siagi, hadi iyeyuke.

Ongeza karoti na kitunguu saumu. Ongeza mchanganyiko wa unga, kwa ule wa maziwa. Ukitumia mikono safi , kanda mchanganyiko hadi uwe laini.

Acha mchanganyiko kwa muda wa saa moja unusu ili uumuke kikamilifu.

Tia mafuta ya kukaanga katika karai.

Tumbukiza kipande kidogo cha kinyunya kwenye mafuta ili kuhakikisha kuwa mafuta yamekuwa moto.

Iwapo hayajapata moto, kipande kitazama kwenye mafuta, na ikiwa yako moto kitaelea juu.

Ukitumia kijiko cha meza, pakua mchanganyiko, huku kijiko kingine kikitumika kuusukuma kwenye mafuta. (Rudia utaratibu huu hadi vipande vya kinyunya vijaze karai).

Kaanga kwa dakika chache, hadi upande wa chini wa mchanganyiko ubadilike na kuwa hudhurungi hafifu.

Pindua kisha uache kwa dakika chache hadi upande huo mwingine uive. (Rudia utaratibu huu hadi vipande vya kinyunya vijaze karai).

Ukitumia kijiko au mwiko toa kaimati zilizoiva kutoka kwenye mafuta kisha uzitie katika chombo kilichotandikwa chachi au karatasi ngumu la unga, ili mafuta yaliyosalia kwenye kaimati yakauke.

  • Tags

You can share this post!

WALIOBOBEA: Haji: Afisa wa utawala na mwanasiasa nguli

MALEZI KIDIJITALI: Likizo ya dijitali hutuliza watoto

T L