MAPISHI KIKWETU: Kuku na supu ya uyoga

MAPISHI KIKWETU: Kuku na supu ya uyoga

NA MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi yenyewe: Dakika 40

Walaji: 3

Vinavyohitajika

  • kuku
  • uyoga kilo 1
  • viazi 4
  • vitunguu maji 2
  • karoti 1.
  • mafuta ya alizeti vijiko 3
  • chumvi
  • maji

Maelekezo

Kwenye maji lita mbili, chemsha kuku kwa dakika 40 kisha epua na uweke kando ipoe.

Wakati nyama hiyo inapoa, chukua uyoga ukate kwa katikati ili uwe na vipande vikubwa. Ikiwa uyoga ni mdogo, usikate.

Katakata vitungu vipande, kisha kwenye sufuria mimina mafuta na yanapochemka, ongeza uyoga na vitunguu kisha ukaange.

Sasa chukua mnofu wa kuku mzima, katakata nyama laini ya kutosha na uitumbukize kwa mchuzi.

Katakata viazi viwe vipande vidogovidogo na ukate karoti. Hivi vyote vitumbukize kwenye mchuzi kisha ongeza chumvi.

Mara tu viazi vitakapoiva – baada ya dakika 20 – ongeza uyoga uliokaanga pamoja na vitunguu kwenye supu. Ache vichemke kwa dakika tatu kabla ya kuepua.

Unaweza kuongezea pilipili unayochuna shambani. Pakua na ufurahie.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge wakataa vipengele kwenye mswada wa fedha...

ZARAA: Wakulima washauriwa wafanye vipimo vya udongo

T L