NA MARGARET MAINA
mwmaina@ke.nationmedia.com
Muda wa kuandaa: Dakika 5
Muda a mapishi: Dakika 20
Walaji: 2
Vinavyohitajika
Utaratibu
Katakata kuku vipande vidogo kisha weka pembeni.
Kaanga minofu hiyo ya kuku kwa dakika tatu kwenye mafuta yaliyoko ndani ya sufuria juu ya moto mkali kisha ongeza sosi ya soya. Punguza moto na endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara, kwa dakika nyingine tatu.
Osha majani ya lettuce vizuri. Kausha na uikate vipande vipande.
Kata nanasi kwa vipande vidogovidogo. Jibini pia inaweza kukatwa au kukwanguliwa.
Changanya mafuta, maji ya limau na pilipili.
Changanya kuku, majani ya lettuce, na vipande vya nanasi kisha mwagilia juu mchanganyiko wa maji ya limau, pilipili na mafuta.
Pakua na ufurahie.