Makala

MAPISHI: Kuku wa kitunguu saumu

March 19th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Saa 12

Muda wa mapishi : Dakika 60

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • Kuku 1
 • Vitunguu saumu 6
 • Mafuta ya mizeituni kikombe 1
 • Thyme kijiko 1 cha chai
 • Chumvi kijiko 1 cha chakula
 • Bay leaf 1
 • Rosemary kijiko 1 cha chai
 • Oregano kijiko 1 cha chai
 • Parsley kijiko 1 cha chai
 • Pilipili vijiko 2 vya chakula
 • Tangawizi kijiko 1 cha chai
 • Vinegar
 • Siagi vijiko 3
 • Vitunguu mboga 2
 • Cornstarch kijiko 1 cha chakula
 • Mdalasini kijiko 1 cha chakula

Maelekezo

Safisha kuku vizuri. Kata vipande vya kawaida kisha mpake chumvi. Hifadhi kwenye chombo pembeni.

Kwenye blenda, weka mafuta ya mizeituni na vitunguu  saumu, thyme, bay, rosemary, oregano, parsley, tangawizi, vinegar, pilipili manga na kitunguu maji.

Saga kwa pamoja hadi mchanganyiko uwe mzito. Toa na weka kwenye chombo pembeni.

Kata kuku vipande vidogo ili kurahisisha viungo kuingia vizuri kwenye nyama.

Mimina mchanganyiko wa viungo kwenye bakuli lenye vipande vya kuku. Changanya vizuri sana hadi vipande vya kuku vilowe.

Toa vipande vya kuku, weka kwenye mfuko kisha funga vizuri na hifadhi kwenye jokofu kwa muda wa usiku kucha.

Ukiwa tayari kumuandaa, toa mfuko. Nyunyizia pilipili na paka unga wa cornstarch juu ya vipande vya nyama.

Pasha ovena nyuzijoto 420°F

Kwenye bakuli la kuokea kwenye ovena, weka foil paper kisha paka siagi juu yake.

Panga vipande vya kuku vizuri kwenye bakuli.

Weka bakuli kwenye ovena kwa dakika 45. Iangalie mara kwa mara kuona kama minofu ya kuku inaiva vizuri na inaungua au la. Geuzageuza.

Chakula kikiwa tayari, pakua na ufurahie na chochote ukipendacho.