Makala

MAPISHI: Makaroni na nyama

April 11th, 2019 2 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 25

Muda wa kupika: dakika 15

Walaji: 2

Vinanyohitajika

 • Makaroni nusu pakiti (pima kulingana na mahitaji yako)
 • Nyanya 4
 • Nyanya ya kopo (tomato paste) vijiko 3
 • Vitunguu maji 2
 • Kitunguu saumu 1
 • Pilipili mboga 1
 • Soy sauce kwa kijiko kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Giligilani kijiko 1 kikubwa
 • Gharam masala ¼ kijiko kidogo
 • Binzari kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi ½ kijiko kidogo
 • Nazi 1 iliyokomaa
 • Njegere glasi 1
 • Biringani 1, kate vipande virefu na vyembamba
 • Italian seasoning kijiko 1 kidogo
 • Pilipili ndefu 2; kata vipande vidogovidogo
 • Cayenne pepper yaani udaha kijiko 1 kidogo

Maelekezo

 • Andaa viungo – menya nyanya, vitunguu maji viwili, pilipili mboga na kitunguu saumu. Kata vipande vidogo. Kamua tui la nazi.
 • Andaa njegere, zichemshe ila zisiive sana. Epua.
 • Kwenye sufuria, weka maji na chumvi, acha yachemke.
 • Weka makaroni, pika kwa dakika 10 kisha epua.  (fuata muda elekezi kwenye paketi ya makaroni)
 • Chuja maji, hifadhi.
 • Ni vizuri ukipika makaroni dakika moja au mbili chini ya muda elekezi kwenye paketi, hii itafanya makaroni yaive vizuri yakichanganywa na sauce na wakati wa kumalizia kupika.
 • Weka mafuta ya kupikia kwenye sufuria, bandika jikoni.
 • Acha mafuta yapate moto vizuri kisha weka kitunguu maji. Hakikisha moto ni mkali ili mboga ziive vizuri bila kuchuja maji.
 • Pika kwa dakika mbili huku unakoroga.
 • Weka kitunguu saumu, bizari, tangawizi, pilipili ndefu, giligilani ya unga, italian season na gharam masala.
 • Koroga vizuri kisha weka nyanya. Koroga taratibu kisha acha ziive hadi zitengane na mafuta. Weka nyanya ya kopo (tomato paste) na biringani na ukoroge pamoja.
 • Weka njegere, koroga pamoja. Weka soy sauce pamoja na chumvi kiasi.
 • Weka makaroni kwenye sufuria. Changanya na sauce ya nyanya na njegere. Weka pilipili mboga, koroga na acha ziive kiasi, ili harufu iwe tamu na nzuri. Weka tui la nazi.
 • Geuza mara kwa mara kisha acha chakula kichemke kidogo. Nyunyizia cayenne pepper na pilipili manga ichanganye na chakula kisha epua.

Chakula kikishakuwa tayari, pakua na ufurahie.