Makala

MAPISHI: Minofu ya kuku

May 14th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 20
Muda wa ku-marinate: Saa 2
Muda wa kupika: Nusu saa

Vinavyohitajika

  • Minofu ya kuku nusu kilo
  • Kijiko 1½ cha kitunguu saumu na tangawizi
  • Vijiko 2 mafuta kwa ajili ya ku-marinate
  • Vijiko 2 mafuta ya kukaangia
  • Red chilli flakes nusu kijiko
  • Chumvi na pilipili ya kutosha
  • Kijiko 1½ cha chicken bouillon powder

Maelekezo

Ichanje kuku iwe na sehemu za kutosha viungo kuingia.

Nyama ya kuku ikiwa mbichi bado. Picha/ Margaret Maina

Kwenye kijibakuli, changanya chicken bouillon powder, mafuta vijiko viwili, red chilli flakes, chumvi, pilipili, kitunguu saumu na tangawizi.

Weka kuku kwenye bakuli kubwa.

Ongeza mchanganyiko wa viungo. Changanya vizuri viungo hivi vikolee kwenye minofu.

Funika bakuli kisha weka kwenye jokofu kwa muda wa saa mbili.

Weka kuku kwenye kikaangio chenye vijiko viwili vya mafuta yaliyochemka katika moto wa wastani.

Acha nyama hii ya kuku iive upande mmoja hadi iwe na rangi ya kahawia, lakini isiungue.

Nyama ya kuku ikiwa imeshaiva. Picha/ Margaret Maina

Geuza upande wa pili, acha ipikike hadi iive vizuri bila kukauka sana.

Pakua mlo huu ungali moto na ambatanisha na chakula kingine utakachopenda; au acha nyama hii ya kuku ipoe kiasi kama utatumia salad.