Makala

MAPISHI: Muffins

June 4th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 30

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 5

Vinavyohitajika

· unga wa ngano gramu 400

· sukari

· baking powder kijiko kimoja

· baking soda nusu kijiko

· chumvi robo kijiko

· mafuta ya kupikia

· ndizi sita mbivu; zigandishe kwenye jokovu

· vanilla essence nusu kijiko

· korosho au karanga za kuoka

Muffins. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

· Washa ovena yako katika moto wa nyuzi 350.

· Chukua chombo cha kuokea yenye mashimo 12 ya queencake kisha weka zile karatasi maalumu za kuokea

· Chukua bakuli safi kavu kisha changanya Uunga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi.

· Kisha toa ndizi zilizokua katika jokovu ziweke kando kwa dakika 20 zitoe barafu.

· Menya ndizi na ziweke kwenye blenda kisha saga mpaka upate rojo.

· Kisha mwagia mchanganyiko wako wa ndizi kwenye mchanganyiko wa unga pamoja na mafuta ya karanga na vanilla.

· Tumia mwiko kuchanganya polepole mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.

· Chukua kijiko kikubwa au mwiko kisha anza kumimina mchanganyiko wako kwenye mashimo ya queencake.

· Oka kwa dakika 30.

· Zitoe muffins zako zikiwa bado katika zile karatasi maalumu za kuokea na weka zipoe

Pakua na ufurahie.