Makala

MAPISHI NA UOKAJI: Biskuti

June 1st, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • unga wa ngano kikombe kimoja na nusu
  • siagi vijiko 4
  • sukari vijiko 6
  • yai
  • vanilla extract
  • baking soda kijiko kidogo
Maumbo ya biskuti tayari kuokwa. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Weka Siagi kwenye bakuli lako la kukandia.

Weka sukari na uanze kuchanganya kwa ama kijiko au mwiko hadi vichanganyike kabisa.

Pasulia yai humo na uchanganye hadi iwe laini itoe kama povu.

Ongeza unga na uchanganye hadi vichanganyike kabisa.

Weka flavour yako kama vanilla au yoyote ile upendayo.

Ukishachanganya kila kitu weka kwenye jokovu kwa muda wa nusu saa.

Washa ovena kiwango cha nyuzijoto 150

Toa unga kutoka kwenye jokovu. Changanya unga wako kwa mkono kisha usukume kwenye kibao na ukate kwa shepu au maumbo mbalimbali.

Panga vipande vyako ulivyokata kwenye chombo cha kuokea.

Oka biskuti zako kwa muda wa dakika 25-30.

Toa biskuti zako; ziache zipoe.

Pakua na ufurahie na maziwa, juisi, chai au chochote ukipendacho.