Makala

MAPISHI NA UOKAJI: Jinsi ya kuandaa tosti zenye ndizi

August 14th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 4

KWA kawaida tosti za mkate hutengenezwa kwa kuchoma vipande vya mkate wa boflo katika kichomeo ili viwe vigumu kidogo.

Vinavyohitajika

· Ndizi mbivu 1 kubwa

· Mayai 2

· Slesi 4 kubwa za mkate

· Kijiko ¼ cha tangawizi ya unga

· Kijiko ½ cha mdalasini ya unga

· Kijiko ½ cha vanilla extract

· Chumvi

· Mafuta ya kupikia

Maelekezo

Ponda ndizi mpaka zilainike vizuri kwa kutumia uma.

Ongeza mayai, mdalasini, tangawizi, vanilla na chumvi. Changanya vizuri.

Paka siagi kiasi kwenye kikaangio katika moto wa wastani. Loweka mkate kwenye mchanganyiko wa ndizi na mayai hadi ukolee vizuri.

Weka mkate kwenye kikaangio. Pika pande zote mpaka ziwe na rangi ya kahawia ila mkate usikauke wala kuungua.

Pakua chakula chako kingali moto.

Furahia na maziwa, juisi au chai.