Makala

MAPISHI NA UOKAJI: Jinsi ya kuoka keki ya jibini iliyo na caramel

November 7th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kuoka: Dakika 45

Walaji: 2

Keki. Picha/ Margaret Maina

Vinavyohitajika

· Cream cheese gramu 400

· Sukari kikombe ½

· Siagi nusu kikombe

· Graham cracker crumbs vikombe 2 (hizi ni kama biskuti)

· Mayai 3

· Vanila vijiko 2

· Caramel cubes kikombe 1

· Caramel sauce nusu kikombe

· Maziwa vijiko 5

· Unga wa ngano vijiko 2

Maelekezo

Pasha ovena nyuzijoto 175. Paka mafuta chombo unachotumia kuokea.

Chukua graham cracker weka kwenye blenda na sukari vijiko viwili halafu saga mpaka ilainike. Pima vikombe viwili.

Chukua bakuli weka graham cracker uliyosaga halafu ongeza hapo siagi. Koroga ichanganyike vizuri kisha weka kwenye chombo cha kuokea. Sasa weka hapo cubes za caramel na uoke kwa dakika 30.

Itoe na iache ipoe.

Chukua bakuli weka cream cheese, mayai, vanila, sukari na unga vijiko 2 changanya mpaka ilainike vizuri, kisha mwagia kwenye ule mchanganyiko ulio uoka mwanzo.

Chukua caramel weka maziwa halafu bandika mekoni. Weka moto mdogo sana kisha mwagia juu ya ule mchanganyiko.

Pakua na ufurahie.