Makala

MAPISHI NA UOKAJI: Mkate wa boflo

January 27th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Saa 2

Muda wa kuoka: Dakika 40

Walaji: 4

Vinavyohitajika

• unga wa ngano kilo 1

• hamira kijiko 1

• chumvi kijiko ½

• sukari kijiko 1

• maziwa

• vanilla kijiko ½

• siagi kijiko 1

• mafuta ya kupikia

Unga wa ngano. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Andaa maji fufutende nusu kikombe.

Weka hamira kwenye maji hayo kisha funika kwa muda wa dakika tano.

Andaa unga wa ngano.

Pasha moto sufuria ya kukandia.

Chemsha mafuta ya kupikia.

Weka hamira (iliyoumuka kwenye maji) kwenye unga. Changanya vizuri kisha mimina mchanganyiko kwenye mafuta yanayochemka.

Koroga kwa kutumia mwiko, japokuwa ni vizuri sana ukitumia mkono (kuwa makini mafuta yasiwe ya moto sana).

Ongeza maziwa huku ukiendelea kukanda hadi unga uwe laini.

Weka siagi kidogo kisha endelea kukanda.

Weka vanilla kisha endelea kukanda.

Paka sufuria mafuta; weka mchanganyiko wa unga uliokanda kisha funika na weka sehemu yenye joto kwa nusu saa ili unga uumuke vizuri.

Mchanganyiko wa unga wenye hamira ukishaumuka vizuri, kanda tena kiasi na kisha gawa matonge madogo madogo (kutegemea umbo utakalo).

Yapange kwenye chombo cha kuokea ambacho umepaka siagi.

Weka kwenye ovena ioke kwa dakika 40 katika nyuzi baina ya 80°C hadi 120°C

Ukifunua na kuona matonge yamebadilika rangi na kuwa kahawia, paka siagi kwa juu na funika. Baada ya dakika mbili, epua na uache mikate ipoe.

Pakua kwa chai, maziwa, kahawa, vinywaji tofauti.