Makala

MAPISHI: Pancakes

April 17th, 2019 1 min read

MUDA wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Mlo wa asubuhi ama kiamsha kinywa ni wa muhimu sana. Watu wengi hufurahia kula pancakes kama kiamsha kinywa. Ni rahisi kuandaa na hazichukui muda mrefu wa mwandaaji.

Vinavyohitajika

  • Vikombe 3 vya unga wa ngano
  • Kijiko 1 cha baking powder
  • Kijiko ¼  cha baking soda
  • Kijiko ¼  cha chumvi
  • Kikombe 1 cha maziwa
  • Kikombe ¼  sukari
  • Yai 1
  • Kijiko 1 cha vanilla extract
  • Kikombe ¼ siagi iliyoyeyushwa
  • Mdalasini kijiko 1 cha chai

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa changanya unga wa ngano, cocoa powder, baking soda, baking powder, chumvi na sukari. Changanya vizuri.

Hatua ya mwanzo kabisa ya kuandaa pancakes. Picha/ Margaret Maina

Kwenye bakuli jingine, changanya maziwa, siagi iliyoyeyushwa, yai na vanilla extract mpaka ichanganyike vizuri.

Chukua mchanganyiko wenye maziwa, mimina kwenye mchanganyiko wenye unga. Sasa changanya vizuri hakikisha hauwi mzito sana wala mwepesi sana.

Kwenye kikaangio kisichoshika chini (non-stick), katika moto wa chini, mwagia unga kiasi cha robo kikombe. Pika mpaka upande wa chini uwe kahawia kwa mbali, na pancake itune kwa juu.

Pancake. Picha/ Margaret Maina

Geuza upande wa pili kisha upake siagi upande wa juu ulioiva. Geuza. Paka siagi hasa upande wa chini. Pika mpaka iive vizuri.

Rudia kwa unga uliobakia mpaka umalize zote.

Pancake. Picha/ Margaret Maina

Pakua na ufurahie na kiteremshio ukipendacho

Pancakes. Picha/ Margaret Maina