Makala

MAPISHI: Samaki wa kuokwa

May 23rd, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

MUDA wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa kuoka: Dakika 45

Walaji : 3

Vinavyohitajika

  • Samaki 3
  • Kitunguu saumu
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Limau au ndimu 1
  • Pilipili
  • Tangawizi 1
  • Vitunguu mboga 2
  • Ndizi 2
  • Mafuta ya mdalasini (Olive oil)
Samaki. Picha/ Margaret Maina

Utaratibu

Andaa samaki kwa kutoa utumbo, magamba na kuosha vizuri. Weka kwenye chombo kikavu pembeni. Ni vizuri na rahisi kama utatumia bakuli la kuokea kwenye ovena.

Inyunyize juisi ya limau vizuri juu ya samaki, nje na ndani kwa uwiano ulio sawa ili samaki apate ladha nzuri ya limau au ndimu atakapokuwa ashaokwa.

Nyunyiza chumvi vizuri nje na ndani.

Ponda kitunguu saumu kisha paka juu ya samaki vizuri; nje na ndani.

Nyunyizia pilipili ya unga juu yake na mpake ndani pia. Hakikisha unatia kiungo hiki kama unakula pilipili. Kama hutumii pilipili hii hatua si lazima.

Weka tangawizi kwenye samaki. Paka vizuri kwa nje na ndani.

Menya ndizi na kisha kata vipande na weka kwenye bakuli lenye samaki.

Kata vitunguu, weka pamoja na samaki. Ni vizuri kama utamuweka samaki juu ya vitunguu ili iwe rahisi majimaji yakichuja yanavidondokea vitunguu.

Nyunziza mafuta ya mizeituni kiasi, kisha paka vizuri kwenye vitunguu pamoja na samaki. Mafuta ni muhimu ili kusaidia samaki aive vizuri bila kuungua. Hakikisha humimini mafuta mengi.

Hifadhi samaki vizuri ili viungo vipate kuingia au kukolea barabara. Inaweza kuwa angalau dakika 45 hadi muda wa saa moja.

Baada ya muda wa saa moja, washa ovena kwenye nyuzijoto 250°C na acha ipate moto kwa takribani dakika 10.

Weka samaki kwenye ovena na uoke kwa muda wa dakika 45.

Mara kwa mara hakikisha samaki chakula hiki hakiungui. Geuza kuzuia kuungua.

Baada ya samaki kuiva, pakua au tenga chakula tayari kuliwa.