Makala

MAPISHI: Scones zilizotiwa juisi ya limau

July 6th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • sukari nusu kikombe
  • kijiko 1 cha maganda ya limau
  • vikombe 3 unga wa ngano
  • baking powder kijiko 1 cha chakula
  • chumvi kiasi cha robo tatu ya kijiko
  • cream cheese kiasi cha robo kikombe
  • vijiko 6 vya siagi (unsalted butter)
  • mayai 2
  • maziwa nusu kikombe
  • kijiko 1 cha juisi ya limau

Maelekezo

Washa ovena na dhibiti kiwango cha joto kiwe ni nyuzijoto 200. Acha ipate moto. Kwangua maganda ya limau na kukamua maji yake.

Katakata siagi iwe vipande vidogovidogo.

Kwa kutumua vidole vyako, changanya uwe kama unasugua sukari na maganda ya limau mpaka ichanganyike vizuri na ilainike.

Ongeza unga wa ngano, baking powder na chumvi. Changanya vizuri.

Katika bakuli jingine, saga cream cheese, siagi na mayai kisha changanya vizuri.

Ongeza mchanganyiko kwenye bakuli lenye unga wa ngano, pamoja na maziwa na juisi ya limau.

Kanda unga mpaka ulainike, kisha katakata kama utakavyopenda.

Unga wa ngano pamoja na viungo vingine tayari umekandwa na kukatwakatwa. Picha/ Margaret Maina

Oka scones kwenye chombo cha kuokea kwa robo saa.

Acha zipoe kwenye waya wa kupozea chakula.

Scones katika waya wa kupoza chakula. Picha/ Margaret Maina

Wakati zinapoa, changanya icing sugar, maji ya limau na maganda ya limau mpaka upate mchanganyiko mzuri.

Scones zikiwa tayari zimepoa. Picha/ Margaret Maina

Nyunyizia mchanganyiko wa icing sugar juu ya scones.

Pakua na ufurahie.