Makala

MAPISHI: Spaghetti na nyama iliyosagwa

March 7th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa kupika: Nusu saa

Walaji: 3

Spaghetti na kima. Picha/ Margaret Maina

Unahitaji

 • Spaghetti gramu 500
 • Pilipili manga
 • Chumvi
 • Siagi kijiko 1
 • Nyama ya kusaga nusu kilo
 • Kitunguu maji 1
 • Pilipili mboga 2
 • Nyanya 2
 • Tangawizi nusu kijiko
 • Karoti 1
 • Curry powder

Maelekezo

Bandika sufuria kwenye meko. Weka maji na chumvi. Ongeza pilipili manga iliyosagwa.

Maji yakichemka weka spaghetti, ziache mpaka ziive kisha chuja maji yote yaishe.

Kwenye sufuria nyingine, weka siagi. Ikishayeyuka weka spaghetti ulilzozichemsha. Changanya vizuri kisha epua.

Weka sufuria nyingine mekoni na ongeza nyama, chumvi, tangawizi na vitunguu saumu. Koroga.

Weka maji ya moto unapoona nyama inakauka. Hakikisha nyama imeiva vizuri; epua na weka pembeni.

Weka sufuria nyingine mekoni, tia mafuta, chumvi kidogo na kitunguu maji. Weka pilipili, na karoti. Koroga kisha weka pilipili mboga na endelea kukoroga.

Weka nyanya, na curry powder. Funika ili nyanya ziive ili kutengeneza mchuzi.

Ongeza nyama kwenye mchanganyiko ule wa nyanya, ongeza Royco. Endelea kukoroga.

Pakua na ufurahie.