Makala

MAPISHI: Wali uliochanganywa na kuku

June 28th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

Minofu ya kuku

Wali uliopikwa

Mafuta ya kupikia

Kitunguu maji

Karoti

Pilipili mboga

Bizari

Pilipili

Chumvi

Njegere

Maji

Mayai

Soy sause

Vitunguu kadhaa vya majani

Maelekezo

Ama upike wali au unaweza kutumia wali uliobaki siku iliyopita (kiporo).

Tengeneza kuku. Kama nyama ya kuku ina mifupa, tenganisha minofu kisha kata vipande vidogovidogo.

Changanya vipande vya kuku na pilipili manga, bizari na chumvi.

Weka kikaangio mekoni kisha kaanga kuku hadi awe kahawia. Akiiva, epua na ufunike vizuri asipoe.

Kwenye sufuria nyingine, weka kitunguu maji, kitunguu saumu, njegere, pilipili mboga, na karoti. Koroga kwa muda wa dakika mbili.

Pasua mayai, mwagia kwenye mboga kisha koroga haraka haraka ili vichanganyike vizuri.

Ongeza mafuta kidogo kwenye mboga.

Weka wali kwenye mboga. Koroga ili uchanganyikane na mboga. Weka kuku, endelea kukoroga kama dakika tano.

Ongeza soy sause kwenye chakula, koroga vizuri ichanganyikane na chakula mpaka maji maji yakauke kwenye chakula na wali uwe na rangi ya kahawia.

Katia vitunguu vya majani kwa juu kisha epua.

Pakua na ufurahie