Makala

MAPISHI: Wali uliokaangwa na kuku

May 15th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa kupika: Dakika 20

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • Minofu ya kuku
 • Wali uliopikwa (Kiporo)
 • Mafuta ya kupikia
 • Kitunguu maji
 • Karoti
 • Pilipili mboga (wengine wanaiita pilipili hoho)
 • Bizari
 • Pilipili
 • Chumvi
 • Njegere
 • Maji
 • Mayai
 • Soy sauce
 • Vitunguu vya kijani

Maelekezo

Pika wali kisha weka kwenye jokofu. Ama kama una wali uliobaki siku iliyopita (kiporo), basi unaweza kuutumia.

Tengeneza kuku kwa kukata vipande vidogovidogo.

Changanya vipande vya kuku na pilipili, bizari na chumvi.

Kaanga kuku hadi awe kahawia. Akiiva, weka pembeni na funika vizuri asipoe.

Kuku. Picha/ Margaret Maina

Bandika sufuria mekoni.

Weka kitunguu maji, kitunguu saumu, njegere, pilipili na karoti. Koroga kwa muda wa dakika mbili.

Pasua mayai, mwagia kwenye mboga kisha koroga haraka haraka ili vichanganyike vizuri.

Ongeza mafuta kidogo kwenye mboga.

Weka wali kwenye mboga. Koroga ili uchanganyikane na mboga. Weka kuku, endelea kukoroga kwa dakika tatu.

Wali. Picha/ Margaret Maina

Ongeza soy sauce kwenye chakula, koroga vizuri ichanganyikane na chakula mpaka maji yakauke kwenye chakula na wali uwe na rangi ya kahawia.

Katia vitunguu vya majani ndani ya mlo.

Pakua na ufurahie mlo wako.