Maradhi Ya Kutatizwa Na Figo yaongezeka nchini

Maradhi Ya Kutatizwa Na Figo yaongezeka nchini

Na LAWRENCE ONGARO

MAGONJWA mengi tunayoshuhudia siku hizo husababishwa na aina ya chakula tunachokila na mpangilio wetu wa kimaisha.

Dkt Elizabeth Wangari wa hospitali ya (Thika Dialysis Centre), alisema baadhi ya chakula tofauti tunayotumia huwa yanachangia magonjwa kama ya figo, kisukari na damu kuchemka.

Hospitali ya Thika Dialysis Centre, ilifunguliwa miaka miwili iliyopita huku ikiwa na nafasi ya wagonjwa 36 kwa wakati moja.

Alitoa mwito kwa wananchi popote walipo wazingatie kupata bima ya hospitali ya NHIF ili wakati wanapoletwa hospitalini kwa magonjwa ya figo kuwe na uwezekano wa kulipiwa gharama ya matibabu.

” Ningetaka kutoa mwito kwa wananchi wachunge miili yao kwa kujua ni chakula yapi wanachostahili kula bila kudhuru mwili,” alifafanua.

Alitoa mwito kwa wananchi wazingatie kufanya mazoezi kila mara na kunywa maji mengi ili kuweka miili yao katika hali bora.

Alisema kipindi cha covi-19 cha awamu ya kwanza wagonjwa wengi wanaougua maradhi ya figo walikuwa na wakati mgumu kwa sababu ya kutafuta matibabu, baada ya sheria ya kusafiri kusitishwa.

” Wakati huu homa ya covid-19, imeshika kasi wananchi wanastahili kufuata maagizo ya wizara ya Afya,” alisema Dkt Wangari.

Mbunge wa Thika Bw Patrick Wainaina, aliyezuru kituo hicho aliridhishwa na vifaa vinavyopatikana hapo akitaja kama hatua nzuri.

” Ninawahimiza wagonjwa wengi ambao hupanga kusafiri hadi nchi za nje kama India wazuru kituo hicho ili waweze kujionea ubora wake,” alisema Bw Wainaina.

Aliyasema hayo jumatano alipozuru kituo hicho ili kujionea mwenyewe jinsi inavyoendesha shughuli zake.

Alitoa mwito kwa serikali kuisaidia hospitali za kibinafsi zinazoonyesha uwezo wa kujiendeleza na kuboresha Afya ya wagonjwa.

Alisema mji wa Thika umebahatika kupata hospitali ya kipekee ambayo ina vifaa vya kisasa vinavyotibu kikamilifu magonjwa na figo na kuosha damu mwilini.

Aliwahimiza wananchi wawe makini na ulaji wao wa chakula kwa sababu ndicho kinasababisha maradhi mengi kuingia miilini mwetu.

” Tungetaka wawekezaji wengi kujitokeza ili kufungua vituo kadha vya kutibu wagonjwa wenye matatizo ya figo kwa sababu ni wengi hapa nchini,” alisema Bw Waiaina.

  • Tags

You can share this post!

IEBC yaidhinisha wawaniaji 6 wa ubunge Juja

MUTUA AMTIA UHURU PRESHA