Habari Mseto

Maraga akataa kuwasimamisha kazi majaji

August 18th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Mahakama kuu Jumanne ilikataa kumzima Jaji Mkuu David Maraga kuwasimamisha kazi majaji na mahakimu waliohudumu kwa muda mrefu.

Jaji Maureen Onyango alisema ombi hilo la chama cha majaji na mahakimu (MJA) halina mashiko ya kisheria.

Chama hicho cha MJA kilikuwa kimemshtaki Jaji Maraga na chama cha kuwaajiri watumisji idara ya mahakama JSC. Kiliomba mamlaka ya kuwasimamisha kazi mahakimu na majaji kwa vipindi virefu vitangazwe kuwa ukiukaji na ukandamizaji wa haki za majaji na mahakimu wahusika.

MJA kiliomba mahakama iamuru muda wa kumsimamisha jaji ama hakimu anayeshukiwa kuwa na utovu wa nidhamu ujulikane ndipo wahasiriwa wasikae manyumbani mwao pasikujua kitakachowavika.

Akitoa uamuzi Jaji Onyango wa mahakama ya kuamua mizozo ya wafanyazi- ELRC- alisema mamlaka ya kusimamisha kazi watumishi wa idara ya mahakama ni JSC ambalo mwenyekiti wake ni Jaji Mkuu (CJ) aliyepia rais wa Mahakama ya juu.

Jaji Onyango alisema suala la kuwachukulia majaji na mahakimu hatua za kinidhamu ni hatua za kiifisi na wala sio hatua ya kinidhamu.

Pia aliamuru JSC itekeleze majukumu yake ipasavyo.