Marefa wa kike kusimamia mechi ya wanasoka wa kiume kutoka Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia

Marefa wa kike kusimamia mechi ya wanasoka wa kiume kutoka Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia

Na MASHIRIKA

WAAMUZI wote watakaosimamia mechi ya kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia za 2022 kati ya Uingereza na Andorra watakuwa wanawake.

Kateryana Monzul kutoka Ukraine atakuwa refa wa kupuliza kipenga katikati ya uwanja huku akisaidiwa na Maryna Striletska na Svitlana Grushko ambao pia ni raia wa Ukraine.

Stephanie Frappart kutoka Ufaransa atakuwa refa wa kusimamia kiwambo cha teknolojia ya VAR.

Itakuwa mara ya kwanza kwa mechi ya haiba kubwa inayohusisha wanasoka wa timu ya taifa ya Uingereza kusimamiwa na marefa wa kike.

Wanaume wawili watakuwa wasimamizi wa ziada wa mechi hiyo itakayoshuhudia Denys Shurman akiwa afisa wa nne wa mechi huku Viktor Matyash akiwa msaidizi wa VAR.

Monzul, 40, alisimamia mechi ya UEFA Nations League kati ya San Marino na Gibraltar mwaka uliopita. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa mechi ya kimataifa ya wanaume kusimamiwa na waamuzi wa kike.

Mnamo 2016, aliweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kusimamia mechi ya haiba kubwa miongoni mwa wanaume nchini Ukraine kabla ya kuwa refa mkuu kwenye fainali za Kombe la Dunia za Wanawake na Soka ya Bara Ulaya kwa Wanawake.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

MKF yasema haijaamua ni nani itaunga mkono

KINYUA BIN KING’ORI: Vita dhidi ya jinamizi la...