Michezo

Mario Gotze apata hifadhi kambini mwa Ajax nchini Uholanzi

October 7th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

PSV Eindhoven kutoka Uholanzi wamemsajili aliyekuwa kiungo matata wa Borussia Dortmund, Mario Gotze kwa mkataba wa miaka miwili bila ada yoyote.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ndiye aliyefunga bao lililowapa Ujerumani ubingwa wa Kombe la Dunia fainali hizo zilipoandaliwa nchini Brazil mnamo 2014.

“Nilipokea ofa nyingi muhula huu. Hata hivyo, maamuzi ya kuteua wapi pa kuelekea yalikuwa rahisi kufanya. Niltaka changamoto mpya na ninahisi kwamba Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) ndiyo yenye kunipa changamoto hiyo,” akasema.

Gotze aliwajibishwa na Dortmund mara 21 katika kampeni za msimu uliopita wa 2019-20 na akawafungia miamba hao wa soka ya Ujerumani jumla ya mabao matatu.

Kabla ya kurejea Dortmund aliowashindia mataji mawili ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Gotze aliwahi pia kuchezea Bayern Munich na kuwanyanyulia mataji matatu ya Bundesliga.

Mbali na Ajax, Mkurugenzi wa Spoti kambini mwa Dortmund, Michael Zorc, amethibitisha kwamba huduma za Gotze zilikuwa pia zikiwaniwa na Liverpool, Bayer Leverkusen na AC Milan.

Hadi kuondoka kwake, Gotze alikuwa amewajibishwa na Dortmund katika jumla ya mechi 201 japo akapangwa katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo mara mitano pekee katika kampeni za Bundesliga mnamo 2019-20.