Martinelli sasa kuchezea Arsenal hadi mwaka wa 2027

Martinelli sasa kuchezea Arsenal hadi mwaka wa 2027

Na MASHIRIKA

FOWADI wa Arsenal, Gabriel Martinelli, 21, ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu utakaomdumisha uwanjani Emirates hadi mwaka wa 2027.

Nyota huyo raia wa Brazil alijiunga na Arsenal mnamo 2019 baada ya kuagana na kikosi cha Ituano nchini Brazil. Tangu wakati huo, amesakatia Arsenal jumla ya michuano 111.

Amepachikia miamba hao mabao saba katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu na kuwasaidia kudhibiti kilele cha jedwali kwa alama 50, tano zaidi kuliko nambari mbili na mabingwa watetezi Manchester City.

Martinelli alichezea chipukizi wa U-23 nchini Brazil mara nane kabla ya kuanza kuwajibikia kikosi cha watu wazima mnamo Machi 2022. Alikuwa sehemu ya kikosi kilichotegemewa na Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar na akachezeshwa na kikosi hicho mara mbili kabla ya kubanduliwa kwenye hatua ya robo-fainali.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

KWPL: Ulinzi Starlets wapiga Vihiga Queens 3-2 uwanjani...

Manchester United wazamisha Palace katika EPL ugani Old...

T L