Mary Wambui apata kazi nyingine serikalini

Mary Wambui apata kazi nyingine serikalini

Na STEVE OTIENO

ALIYEKUWA Mbunge wa Othaya, Bi Mary Wambui, sasa ndiye mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Hazina ya urekebishaji tabia za familia zinazorandaranda mtaani (chokoraa).

Amechukua mahali pa aliyekuwa Mbunge wa Marakwet Mashariki, Bi Linah Jebii Kilimo. Bi Wambui atatumikia wadhifa huo kwa miaka mitatu.

Waziri wa Leba, Bw Simon Chelugui, alitangaza mabadiliko hayo kwenye gazeti la serikali lililochapishwa Ijumaa.

Mnamo Januari 2020, mahakama ya masuala ya ajira ilifutilia mbali uteuzi wa Bi Wambui kama mwenyekiti wa Mamlaka ya Kitaifa ya Ajira (NEA).

Mahakama iliamua hakuajiriwa kwa wadhifa huo kwa njia zinazofaa kwani hakuhitimu kuwa mwenyekiti wa NEA.

Jaji Onesmus Makau alitoa agizo la kudumu kuzuia Bi Wambui asiajiriwe kwa wadhifa huo.

Kesi ilikuwa imewasilishwa na Seneta wa Nairobi, Bw Johnson Sakaja ambaye ndiye alikuwa amefadhili mswada uliopelekea kuundwa kwa NEA.

You can share this post!

Partey kurejea ugani kusaidia Arsenal kuanza kutetea...

Maafisa walaumiwa kwa kupendelea watu wa Trump