Maseneta wagonga mwamba

Maseneta wagonga mwamba

Na RICHARD MUNGUTI

JITIHADA za maseneta kubuni hazina watakayosimamia katika kaunti ziligonga mwamba mahakama ya juu iliposema jana jukumu lao ni kuhakiklsha gatuzi zimesimamiwa vizuri na magavana

Katika uamuzi wake mahakama hii ya upeo jana ilitamatisha mvutano kati ya magavana na maseneta kuhusu usimamizi na matumizi ya pesa zinazopelekwa kugharamia maendeleo. Na wakati huo huo mahakama hiyo ilikataa kubiwa kwa hazina ya kaunti ambayo ingelisimamiwa na maseneta.

Jaji Martha Koome pamoja Jaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Nkoki Ndungu na William Ouko walisema jukumu kuu la Seneti ni kuhakikisha kaunti zimeendelezwa kwa mujibu wa sheria na zimetumia pesa kama ilivyopitishwa na mabunge ya kaunti.

Majaji hao walisema marekebisho ya sheria ambayo seneti ilitaka ungelipelekeakubiwa kwa hazina maalum ya kaunti (CDBs) ambayo wenyeviti wake wangelikuwa Maseneta. Jaji Koome na majaji wanne wa mahakama hii ya upeo walisema kubadilishwa kwa sheria hiyo kuwapa maseneta mamlaka ingelibuniwa tu kupitia kwa kura ya maoni (refereda).

Pia mahakama ilisema kuwa haina wajibu wowote kuwatangaza maseneta kuwa wakuu wa Magavana. Pia walisema maseneta hawana jukumu lolote kuamuliwa kaunti miradi ya maendeleo itakayopewa kipau mbele. Kutupiliwa mbali kwa kesi hii ya maseneta kumetimisha kuwa ya tatu kukataliwa na mahakama hii ya upeo.

Jaji Koome na wenzake walisema kubuniwa kwa CDBs na Bunge la Kitaifa ni ukiukaji wa Katiba Seneti iliwasilisha rufaa hiyo 2019 ikiomba marekebisho ya sheria za kusimamia serikali za kaunti zikubaliwe na zianze kutekelezwa mara moja.

Kupitia marekebisho hayo bodi za CDBs zilitakiwa kubuniwa kutekeleza kazi kama zile za Hazina ya Kustawisha maeneo bunge (CDFs). Seneti iliwasilisha kesi hiyo 2014 na kusikizwa na majaji George Odunga, Mumbi Ngugi na Isaac Lenaola ( alipokuwa jaji mahakama kuu).

Majaji hao walitupilia mbali kesi hiyo wakisema jukumu la maseneta imetangazwa bayana katika katiba kwamba kazi yao ni kutunga sheria za kuthibiti utenda kazi katika magatuzi. Seneti ilikataa rufaa kisha mahakama ya pili kwa ukuu nchini ikakubaliana na uamuzi wa majaji Odunga , Ngugi na Lenaola.

Mahakama hii ya juu ilitupilia mbali rufaa ya seneti. Jaji Koome na wenzake walisema hoja iliyowasilishwa na Seneta Moses Kajwang ya kufanyia marekebisho sheria za ugatuzi utaimbua mabadiliko wanayotazamia.

You can share this post!

Shabiki Isaac Juma azikwa kishujaa Kakamega

Levante yaduwaza miamba Atletico Madrid ligini

T L