Habari MsetoSiasa

Maseneta wenye zaidi ya miaka 58 kufanyia kazi nyumbani

March 31st, 2020 1 min read

NA DAVID MWERE

Spika wa Seneti Ken Lusaka ametangaza hatua zitakazoruhusu maseneta 28 pekee  kuendelea kuhudhuria vikao vya seneti.

Hii, alisema, ni mojawapo ya mbinu za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Maseneta na wafanyakazi wa seneti walio na zaidi ya miaka 58 wameakiwa kufanyia kazi nyumbani kufuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta.

“Ninawarai maseneta wote na wafanyakazi wa afisi za seneti kufuata mwongozo huu ili kutoa fursa kwa mijadala kuendelea huku tukijikinga. Nitatoa maelezo zaidi ikibidi,” Bw Lusaka akasema.

Orodha ya maseneta 28 ilifikiwa wakati wa kutano wa mpingao ya mijadala ya seneti hapo Jumatatu.

Kuwiana na maagizo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), seneti imepunguzwa hadi maseneta wasiozidi 28 kwa vikao vyote vijavyo.

IMETAFSIRIWA NA FAUSTINE NGILA