Michezo

Mashabiki 1,000 kuruhusiwa uwanjani wikendi hii

September 17th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

JUMLA ya mashabiki 1,000 watakubaliwa kuhudhuria mechi 10 tofauti katika soka ya Uingereza wikendi hii kama sehemu ya mpango wa serikali kurejesha mashabiki viwanjani baada ya janga la corona.

Maamuzi hayo ni zao la mashauriano kati ya serikali ya Uingereza na vinara wa soka ya taifa hilo (EFL) huku mashabiki zaidi wakitarajiwa kuhudhuria michuano mbalimbali kuanzia Oktoba 1, 2020.

Hakuna mashabiki wamekubaliwa kuhudhuria mchuano wowote katika soka ya Uingereza tangu Machi 2020 kwa sababu ya hofu ya msambao wa virusi vya corona.

Jumla ya mechi tatu za Daraja la Kwanza (Championship), nne za Ligi ya Daraja la Pili na tatu za Ligi ya Daraja la Tatu zimeteuliwa kwa minajili ya kufanyiwa majaribio ya kuruhusu hadi mashabiki 1,000 kuhudhuria wikendi hii (Jumamosi ya Septemba 19, 2020). Mechi hizo ni kama ifuatavyo:

Championship:

  • Luton Town na Derby County
  • Middlesbrough na AFC Bournemouth
  • Norwich City na Preston North End

League One:

  • Blackpool na Swindon Town
  • Charlton Athletic na Doncaster Rovers
  • Hull City na Crewe Alexandra
  • Shrewsbury Town na Northampton Town

League Two:

  • Carlisle United na Southend United
  • Forest Green Rovers na Bradford City
  • Morecambe na Cambridge United

TAFSIRI: CHRIS ADUNGO