Mashairi

MASHAIRI: TUWE ANGE

April 1st, 2020 4 min read

TUWE ANGE

Sichoki kuambieni, jambo jema la fanaka

Nyote mjiandaeni,yafao kuajibika

Msingoje maishani, kujua ya kuepuka

Sisi sote tuwe ange kufikia lengo letu

 

Kujiepuka mabaya, ni sisi jukumu letu

Tuyatende bila haya, kujimudu jera zetu

Tusiwe wakufanyiya, mzaha maneno yetu

Sisi sote tuwe ange,kufikia lengo letu.

 

Muda twaupoteza, kwa fikra zetu mifu,

Musingoje kupoteza, malengo yenu kwa hofu,

Nia itawaangaza, kwa nuru ya ubinifu

Sisi sote tuwe ange kufikia lengo letu.

 

Wengi nyuma twazembea, kwa hatua twamuayo

Bado jatelekezea, majukumu yataayo

Tuwache kusingizia,wamuzi wangamizao

Sisi sote tuwe ange, kufikia lengo letu.

 

Ni mengi tumeyaona, sharti tuyatelekeze

Singoji kukolezana, ndipo `si tuyadekeze

Mazuri ni kufunzana, mabaya tuyalegeze

Sisi sote tuwe ange, kufikia lengo letu.

 

Tamati nimefikai, ni wazi tuwe tayari

Mwache kulekezea, a wamu ya ushauri

Yote yatafanikia, bora tuwe wamahiri

Sisi sote tuwe ange, kufikia lengo letu.

 

DUNIA MASHAKA MAKUU

Hofu dunia kote, bila nuru kuangaza

Haribifu upo kote, uchao kutekeleza

Uwovu huu wote, ni sisi kuyasambaza

Sisi sote tufahamu, duniani mashakani

 

Masikini kwenye daraja, na wale wenye minofu

Sio wote wana haja, ‘saidizi bila hofu

Kile hicho anacho mja, hana mwenza wadilifu

Sisi sote tufahamu, duniani mashakani.

 

Ja fisi mawindoni, wana mengi ya tama

Ni kwao bila idini, kutosheka kuwania

Maovu ulimwenguni, twatenda ‘sipojali

Sisi sote tufahamu, duniani mashakani.

 

Wengi wetu mepotoka, kupata raha ya dinia

Haya ya kutamanika, mali nyingi ya dunia

Tuliko twasikitika, ‘haribifu bila nia

Sisi sote tufahamu, duniani mashakani.

 

La mbiu nalitia , ninyi kwenu kuamua

Huna budi kuwania, tendea mema dunia

Sisi sote tufahamu, dunia ni mashakani.

 

UFISADI

Limekuwa uonda sugu, laturejesha gizani

Linakua kama mbegu, latunyonya ja kunguni

Limeuvuja udugu, na kutuacha zogani

Wananchi tukuwe macho, kumaliza janga hili.

 

Walio uongozini, ndio wenye usukani

Chakushangaza lakini, ‘macho yao hayaoni

Uovu ulivyo nchini, ‘mekuwa kwao gizani

Wananchi tukuwe macho, kumaliza janga hili.

 

Fedha kuvunjwa na wao, mwananchi kulipa

Wanazijengea kwao, makao ya kuvutia

Kweli hawana wazio, jambo hili ‘endelea

Wananchi tukuwe macho kumaliza janga hili.

 

Wengi weyu ‘mepoteza, mali yetu kiholela

Rushuwa ‘metuangaza, kwa njia ya mulungula

Nastahili kutekeleza, yafaao kijumula

Wananchi tukuwe macho, kumaliza janga hili

 

Viongozi tafadhali, twahitaji haki zetu

Si kila mara ‘tojali kulinda maisha yetu

Tusiwe wa kuhimili, mali zisizo zetu

Wananchi tukuwe macho, kumaliza janga hili.

 

Wakuongoza ni nyie, ni kwenu maendeleo

Ndipo sisi tuchangie, kujenga pafao

Hapo ndipo tuingizie, udugu tuuko sao

Wananchi tukuwe macho, kumaliza janga hili

 

Kalamu naweka chini, ili mnipate nyote

Langu ninawachieni, kutenda udugu kote

Haya yote tendeni, usawa kudumu pote

Wananchi fuwe macho,kumaliza janga hili

 

TENDA HAKI

Una haki kutendewa, hiari

Bila kosa kufanyiwa, hatari

Pawa pote na usawa, hayari

Tenda haki

 

Yako pia yakufika, fikiri

Haki yako utatoka, ukari

Ni wewe kuajibika, jabari

Tenda haki

 

Wangu wako ushauri, hodari

Usiyakose kuyakiri , ayari

Pawe kwako na heri, wa shwari

Tenda haki

 

Kuna watu bila utu, ghururi

Unyama wao kwa watu, hanjari

Jihadhari ja kulunga, hodhari

 

UPENDO

Upendo ni uvumilivu

Upendo sio wivu

Na upendo huna kiburi

Upendo hauna kukasirika

Upendo hauna maudhi

Na upendo haufurahii

Wakati mabaya kutendeka

Upendo kila huaminiwa

Kuwa na tumainina hifadhi

Na upendo kwa kweli

Ni wetu kwetu wa milele

 

NIPASHE

Nitokapo kizuizini

Naomba yeyote kwa undani

Anipashe yaliyo

Anieleze yaliyo

Anifahamishe yaliyo

Taratibu niyapate

Niyasikize haya yote

Nipashe maisha yaliyo

Jinsi waja watakavyo

Nifunze maisha tena

Unijuze haya tena

Unieleze haya tena

Niko hapa tayari

Nimekubali kwa hiyari

Mema haya nafikiri

Nipashe!

Nipashe!

………………..Ibrahim Malili………………Mtunzi

UHURU WETU

Kwetu sisi twajivunia

Uhuru wetu kuwania

Ni mengi tumeyaona

Kwa serikali ya wakoloni

Uhuru ni wetu sote!

Wazungu waende wote!

Tupate mali yetu yote!

Tangu jadi tumedhulumiwa

Unyanyasaji kufanyiwa

Mauwaji kutendewa

Mateso kutelekelezewa

Uhuru ni wetu sote!

Afrika ni yetu sote

Viongozi ni wetu wote!

……………..Ibrahim Malili……………….Mtunzi

 

MULA NAWE HAFI NAWE

Ni kweli nie wosia,kwako wewe kuhofia

Ni vyema kuangazia,yako mema kutendeka

Bila kwenu kuluzia,yafao kuangazia

Muwe ange kuyajua,mulanawe hafi nawe

 

Ni mema mnatenda,kila mara mwasaidiana

Bila kwenu kujitenda,yafao ya rahani

Niye kwenu kuyapenda,fanikio ya hazina

Muwe ange kuyajua,mula nawe hafi nawe

 

Siwe wa kujilaumu,baada ya kupotoka

Ni mwenyewe kujidhumu,maisha haya utaka

Ya mrama bila hamu,ni kwako kusikitika

Muwe ange kuyajua, mula nawe hafi nawe

 

Yaishi maisha yako,ya mwenzio tia komo

Ja kinyonga siwe kwako,kupoteza yaliyomo

Mema kwako yawe uko,uyapate bila zimo

Muwe ange kuyajua,mula nawe hafi nawe

 

Bila muda kupoteza,kwako kutoa wamuzi

Mema kwako kuangazia,kuyatenda yawe wazi

Amulia yakupaza,yakutenda sipo gizi

Muwe ange kuyajua, mula nawe hafi nawe

 

AFRIKA YA WAAFRIKA

Ni ari yenu kufurahia

Kama Afrika kutamania

Kama kwenu kujivunia

Nchizenu kuwania

Sio enzi kamwe ya wakoloni

Kutupa taabu akilini

Wala kutuwacha sisi taabani

Kulia kwetumasikini

Afrika muko na uhuru

Kilamja awe na uhuru

Yote yatendeke ya kuzuru

Kwa haki na uhuru

Tunajiongoza wenyewe sasa

Mfano mwema tuonyeshe hasa

Tuungane bila mikasa

Na tuepuke mabaya anasa

Nchi zote kwa pamoja

Muwe na msingi bila daraja

Kila mwafrika awe mweyehaja

Ya kujenga nchi bila haja

 

HAKI YANGU YA ELIMU

Kijana:Enyi nawauliza,kosa gani na elimu

Kila mara nawajuza,elimu bora hudumu

Ja kinyonga mwapuuza,hatapia kunishtumu

Haki yangu nalilia,bila mali kuwapora

 

Wazazi:Tumekupa kila kitu,wahitaji nini tena

Malezi pasipo kutu,tumekupa ya kufaana

Kazi yako bila utu,kila mara twagombana

Kosa lakoukashifu,litakupa shida wee

 

Kijana:Sisemi kwa ukashifu,nawaheshimu nyi sana

Langu kwenu bila hofu,elimu ya kufaana

Neno langu msadifu,udhuluma usiwe tena

Haki yangu nalilia,bila mali kuwapora

 

Wazazi:Kazi hizi zote zako,uwajiri wako wetu

Mshahara pata wako,kutoka mifuko yetu

Swala hilo si lako,elimu kukosa utu

Kosa lako ukashifu,litakupa shida wee

 

Kijana:Malipo mnanipea,nikweli sijakataa

Mema mwanitendea,sina budi kuhadaa

Kazi ninawafanyia,bila haya mwanipuuza

Haki yangu nalilia,bila mali kuwapora

 

Wazazi:Utaenda skuli vipi,huna hali wala mali

Vitabu upate wapi,vyako vya kuhistimili

Karo utapewa vipi,kwako hilo ni muhali

Kosa lako ukashifu,litakupa shida wee

 

Kijana:Ni kwenu nawaombeni,mnipeleke shuleni

Nakuwana huzuni,kukuwa bila somoni

Uhaba wangu shuleni,telekeza umasikini

Haki yangu nalilia,bila mali kuwapora

 

Wazazi:Ni wazi tumesikia,shuleni takupeleka

Mengi utayasomea,uyapate bila shaka

Tuwie radhi kosea,haki yakokutoweka

Kosa lako ukashifu litakupa shida wee

 

Kijana:Asanteni nashukuru,ombi langu kusikia

Nitasoma bila dhuru,hali yenu angazia

Maisha yawe ya huru,bila hofu kuzindukia

Hakiyangu nalilia,bila mali kuwapora