• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
SHAIRI: Korona kufuli nzito

SHAIRI: Korona kufuli nzito

NA LEVIS TUNJE

Jina ninaitwa Ndoro,  nimekwama chuoni Moi.

Masomo yanakasoro,  Korona yanacha hoi.

Virusi ni minyororo,  shida yangu haipoi

Korona kufuli nzito,  yatufungia masomo.

 

Nimeshindwa kwenda homu,  likizo hi ya lazima.

Ni mbali kwetu ni Lamu,  nauli hakupata mama.

Heri kutuma salamu, kaya kama wa salama.

Korona kufuli nzito,  yatufungia masomo.

 

Twasoma kwenye wavuti,  hatwonani darasani.

Wamekataa umati,  wa wanagenzi chuoni.

Elimu yanilawiti,  Nazekea masomoni.

Korona kufuli nzito,  yatufungia masomo.

 

Mama analalamika,  Biashara hailipi.

‘Kamua kufunga duka, wateja hawamlipi.

Mi sina hata sadaka,  za mlo tapata wapi?

Korona kufuli nzito, yatufungia masomo.

 

Nachukia mwezi machi,  kama tuu mwaka jana.

Hili janga halachi,korona kongezekana.

Mapigo haya ya mchi,  nchini kimeumana.

Korona kufuli nzito,  yatufungia masomo.

 

Malenga: Levis Tunje (malenga mhengah), Kilifi.

You can share this post!

Mafisadi katika utoaji wa chanjo waonywa

Kilichomng’oa Sheffie Weru kazini chapata shahidi...