• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
SHAIRI: Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

SHAIRI: Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

NA ASSUMPTA WAUSI

Dunia maji ya ndimu, ni chungu wewe sikia

Siteti si soga humu, nasema huu wosia

Dunia kama hakimu, uzimlika tabia

Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

 

Wanaume binadamu, wote nawasalimia

Ninayo hii kalamu, hoja kuwaandikia

Kama mama,bintiamu, dada pia malkia

Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

 

Msimamoye heshimu, simlazimishe ndoa

Acha apate elimu, na wosia atakua

Mfunze na ukarimu, asije akapotea

Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

 

Ndugu zangu pesa tamu, kimpa tambugia

Masomoye na walimu, ataacha angalia

Wazazi chemka damu, na ya kesho utaua

Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

 

Mtunze usihukumu, ataongoza mkoa

Mkufunzi na hakimu, iwe ngao na kofia

Ufanisi ni sehemu, yao kwa hii dunia

Msichana ni muhimu, heri kumsaidia.

You can share this post!

Kocha Ronald Koeman wa Barcelona asema amechoka kujitetea...

Tumewafaa wateja wetu wakati wa corona – Safaricom