• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 10:55 AM
SHAIRI: Msirarue maisha yangu

SHAIRI: Msirarue maisha yangu

Nanena nisikike,

Nitambulike nipewe haki yangu,

Hadhi yangu nipate,

Heshima zangu nipokee.

 

Elimu kamwe nisikose,

Shule niende nisibaki nyuma,

Mama, baba, kaka usinitenge,

Shule, msikiti, kanisa, kijiji usiniteme .

 

Babu, nyanya msinioze bado ni mdogo,

Tamaduni zasema mimi mke,

Lakini mimi bado mwanafunzi,

Ulimwengu unakua, nataka kukua.

 

Kidole cha lawama nanyoshewa,

Sikatai yangu makosa,

Mimba kapata ningali mdogo,

Juu ya kidonda msumari.

 

Nikosoe usiniachie ulimwengu,

Walimwengu watanipotosha, ndoa itanimeza,

Thamani yangu haijapungua,

Akili zangu zi timamu.

 

Usikatize masomo yangu nasihi,

Ndoto ya kuwa mwalimu, daktari i hai,

Nyota yangu isizime ing’a,

Maisha yasiraruke ningali mdogo.

 

Na ASSUMPTA WAUSI

#GirlChildVoice.

You can share this post!

Wakazi wa Mombasa wafurahia daraja jipya la kuelea Liwatoni

Wasichana wengi zaidi wakeketwa msimu wa Krismasi