• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 2:08 PM
SHAIRI: Ubakaji kama makaa

SHAIRI: Ubakaji kama makaa

NA ASSUMPTA WAUSI

Kungwi ninayo barua, maisha kisulisuli

Nicheze yangu gitaa, ujumbe ufike mbali

Wifi ,halati bavyaa, mtambue minajili

Ubakaji ja makaa, uchoma tena vikali .

 

Kwa ami kaendelea, kulindwa kama kipuli

Nikaitwa malkia, kajisahau akili

Mtoto sasa nalia, ami kaniumia sili

Ubakaji ja makaa uchoma tena vikali.

 

Somo shangazi kaua, hauoni ufidhuli

Binamuzo nao pia, kauparamia mwili

Hila yote kanivamia, iko wapi serikali

Ubakaji ja makaa, uchoma tena vikali.

 

Nani wakunifidia, donda sawa na kivuli

Yaniuma kila saa, matendo haya katili

Asilimia ni mia, kilio changu ahali

Ubakaji ja makaa, uchoma tena vikali.

 

Yamekuwa mazoea, halati yu pilipili

Jumapili Ijumaa, nawaitaji wakili

Waondoe kitambaa, cheusi cha makali

Ubakaji ja makaa, uchoma tena vikali.

 

 

You can share this post!

Wahalifu watumia maombi kuwahadaa wakazi wa Thika

SHAIRI: Ndoto yangu yazimika