Habari Mseto

Mashakani kwa kuiba nduma za Sh14,000 Kangemi

September 5th, 2018 1 min read

Na Benson Matheka

MWANAMKE alishtakiwa Jumanne kwa kuiba nduma za thamani ya Sh14,000 katika soko la Kangemi jijini Nairobi na kisha akamchapa mlalamishi.

Bi Jane Nakuti alikanusha mashtaka mawili mbele ya Hakimu Mkaazi Mkuu wa Kibera, Bi Faith Mutuku na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh20,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Ilidaiwa kwamba aliiba nduma hizo mali ya Bi Josphine Makichi mnamo Septemba 2 katika soko hilo kwenye barabara ya Waiyaki jijini Nairobi.

Pia alidaiwa kumpiga Bi Makichi na kumsababishia majeraha mwilini. Hata hivyo,aliwachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 pesa taslimu hadi Novemba 22 ambapo kesi hiyo itasikilizwa.