Habari Mseto

Masharti mapya yaliyotangazwa na serikali kuzuia maambukizi ya virusi vya corona

March 20th, 2020 1 min read

Na CHARLES WASONGA

MASHARTI mapya yametangazwa na Serikali, kupitia Wizara ya Afya, Ijumaa ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

A) Baa, kumbi za burudani na vilabu vyafaa vifungwe saa moja na nusu usiku kila siku kuanzia Jumatatu, Machi 23, 2020

B) Maduka yote ya supamaketi yapunguze idadi ya wateja kwa wakati mmoja ili kuzingatia kanuni ya umbali wa mita moja na nusu kati ya mtu mmoja na mwingine. Yahudumu kwa saa 24 na yatapewa ulinzi na serikali.

C) Masoko ya wazi yaendelee kuhudumu lakini yanyunyiziwe dawa kila wakati kudumisha usafi. Misongamano ya watu idhibitiwe.

D) Serikali za kaunti zikusanye takataka katika masoko yote kila siku na zihakikisha kuna maji na sabuni kuwezesha watu kunawa kila mara

E) Kampuni na masharika yawaruhusu wafanyakazi wao wafanye kazi wakiwa nyumbani pale inawezekana.

F) Viwanda viruhusu wafanyakazi wachache kuhudumu kwa wakati mmoja, kwa zamu na kwa saa 24.

G) Magari ya uchukuzi wa umma yapunguze idadi ya abiria.

i) Matuta zenye uwezo wa kubeba abiria 14 zibebe watu wanane pekee.

ii) Yale magari ya abiria 25 yabebe abiria 15.

iii) Magari ya abiria 30 na zaidi na hata treni, zibebe asilimia 60 ya abiria. Kanuni hii pia izingatiwe katika huduma za treni ya SGR

H) Idadi ya wanaowatembelea wagonjwa hospitalini ipunguzwe.

I) Wakenya na wageni waliowasili nchini wajitenge kwa siku 14 kabla ya kuruhusiwa kutangamana na watu wengine.