Mashirika yaitaka serikali iwakabili wafanyabiashara wenye umero

Mashirika yaitaka serikali iwakabili wafanyabiashara wenye umero

Na LEONARD ONYANGO

MASHIRIKA ya kutetea watumiaji wa bidhaa yameitaka serikali kuwakabili wafanyabiashara ‘wajanja’ wanaoongeza kiholela bei ya vyakula na bidhaa nyinginezo muhimu wakati huu wa janga la corona.

Mashirika hayo ya kutetea watumiaji wa bidhaa yanayojumuisha; Consumer Unity and Trust Society (Cuts), Consumer Information Network (CIN), Consumer Grassroot Association, Kenya Consumer Organization (KCO) na Consumer Downtown Association (CDA) jana yalisema kuwa bei ya vyakula na bidhaa nyinginezo muhimu imekuwa ikiongezeka kila uchao na imeanza kulemea idadi kubwa ya Wakenya.

“Uchunguzi tulioufanya umebaini kuwa bei ya vyakula madukani imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miezi mitatu iliyopita. Inasikitisha kuwa bei ya vyakula inapanda licha ya bei ya mafuta kushuka na hata serikali kuruhusu mizigo kuendelea kusafirishwa kote nchini,” akasema Daniel Asher wa shirika la CUTS International.

Bw Asher aliitaka Mamlaka ya Kupambana na Bidhaa Feki (ACA) na Shirika la Kudhibiti Bidhaa (Kebs) kupambana na wafanyabiashara wanaohatarisha maisha ya Wakenya wasio na hatia kwa kuwauzia barakoa na dawa feki za kusafisha mikono.

Baadhi ya maafisa wa kutoka katika mashirika ya kutetea watumiaji bidhaa wakiwahutubia wanahabari jijini Nairobi. Picha/ Leonard Onyango

Mashirika hayo pia yalisema kuwa idadi kubwa ya Wakenya, haswa katika maeneo ya vijijini, hawana ufahamu wa kutosha kuhusu namna ya kujikinga na kujiepusha dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Kulingana nao, Wakenya hawafahamu jinsi ya kutumia na kutumia na kutupa barakoa zilizotumika bila kuhatarisha maisha yao.

“Serikali, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (CA) na Wizara ya Afya (MOH), inafaa kuhakikisha kuwa kuwa wananchi wanapata habari sahihi kuhusu janga la corona,” akasema Bw Japheth Ogutu, mkurugenzi wa shirika la CDA.

You can share this post!

Magoha asisitiza mitihani ya kitaifa ingalipo mwaka huu

Serikali kuwaondoa kwa lazima walioko katika...

adminleo