Masumbwi ya Jamal yang’oa nanga Kisumu

Masumbwi ya Jamal yang’oa nanga Kisumu

Na CHARLES ONGADI

HATIMAYE Shirikisho la Ndondi Nchini (BFK) limetoa ratiba ya mashindano ya President Jamal Boxing Championship yanayong’oa nanga leo mjini Kisumu.

Mashindano yanatarajiwa kuanza rasmi mida ya saa nane kwa mapigano ya muondoano kisha siku ya alhamisi kuandaliwe mapigano ya robo fainali.Kulingana na katibu mpanga ratiba wa BFK, John Waweru, mechi hizo zitatanguliwa na shughuli ya kuwapima afya na uzito mabondia asubuhi.

Kisha mkutano wa kamati ya kiufundi ya BFK mchana, itakayopisha semina ya majaji na marefa wa mashindano.Katika mashindano ya mkondo wa kwanza yaliyoandaliwa Nairobi wiki mbili zilizopita, klabu ya Kenya Police, almaarufu Chafua Chafua, iliibuka kidedea kwa jumla ya alama 25 ikifuatwa na KDF kwa alama 19.

Aidha, mashindano ya leo yanatarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali ikizingatiwa ndiyo ya mwisho mwaka huu.Pia washindi watapata fursa ya kuwakilisha taifa katika michapano ya kimataifa mwaka ujao.Kocha mkuu wa timu ya taifa Musa Benjamin alidokeza kuwa, baada ya mashindano haya atapata nafasi ya kuchagua kikosi imara kwa ngumi za kimataifa 2022.

Police wanaonolewa na kocha David Munuhe, wanatazamiwa kuwa na washiriki wengi katika timu ya taifa kutokana na idadi kubwa ya mabondia wake waliofika fainali za Nairobi.Hata hivyo, watakumbana na upinzani mkali kutoka kwa mahasidi wa jadi KDF, Nairobi, Kongowea na kikosi cha Magereza.

You can share this post!

Cherono sasa alenga taji la Dunia, Madola

Ni kufa au kupona kwa Barca leo UEFA

T L