Habari

Matamshi ya Jaguar yakoroga mambo mataifa jirani

June 26th, 2019 1 min read

Na AMINA WAKO na MASHIRIKA

TANZANIA imemtaka Balozi wa Kenya nchini humo Dan Kazungu kufafanua matamshi dhidi ya wageni wanaoishi nchini Kenya ambayo yalitolewa na mbunge wa Starehe, Charles Njagua akitishia kwamba wataondolewa katika masoko ya miji nchini.

Kwenye video inayoenea katika mitandao ya kijamii, mbunge huyu maarufu ‘Jaguar’ alizungumza kuhusu watu kutoka Tanzania, Uganda, na China akiwasuta kuingilia na hata ‘kutawala’ masoko mengi jijini Nairobi.

Ni katika eneobunge lake ndiko kuna soko maarufu Afrika Mashariki la Gikomba.

Soko hilo ni maarufu kwa mitumba.

“Hapa hatuzungumzii raia sita wa China waliosafirishwa kwao kwa kuuza mitumba. Tunazungumzia mamia ya wageni wanaofanya biashara hapa (Kenya). Ninaipa serikali muda wa saa 24 kuwafurusha wageni hawa, la sivyo nitawakabili wageni hawa kwa kuwaondoa madukani na kuwapeleka katika uwanja wa ndege,” alisema.

Tayari msemaji wa serikali Charles Oguna amesema hayo ni matamshi ya mbunge huyo na kwamba si msimamo wa serikali.

Bunge la Tanzania mnamo Jumanne lilijadili suala hilo ambapo Spika Job Ndugai aliitaka serikali ya Kenya kuwahakikishia raia wa nchi hiyo usalama wao.

Habari kamili inaandaliwa…