Habari Mseto

Matatu zapigwa marufuku katikati ya mji wa Nakuru

September 21st, 2020 1 min read

Na Eric Matara

Matatu hazitaruhusiwa kuingia ndani ya Nakuru kuanzia Jumatatu kwenye juhudi za kaunti hiyo za kupunguza msongamano mjini.

Matatu hizo zilikuwa zimetolewa mjini mwezi machi kwenye juhudi za kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Gavana Lee Kinyanjui amepiga marufuku usafiri wa magari ya umma kutoka mjini Nakuru.

“Tumeamua hakuna matatu itaruhusiwa katikati mwa mji Nakuru,”alisema kwenye uziduzi wa mpango wa miaka tano wa hospitali ya Our mjini Nakuru.

“Mpango huo utawezesha ukuzi wa mji wetu.Maafisa wangu watahakikisha kwamba waendesha matatu wamerithishw na mahala wametengewa.Tutahakisha kwamba kituo hicho ch matatu kina maji na vyoo.”

Hii inamaanisha kwamba wasafiri watalazimika kutembea kwa umbali kutoka mjini ili kuchukua matatu nje ya mji wa Nakuru.

Magari ambayo yatahadhirika ni ya, Prestige shuttle , 2NK, Nyakakima Line, Nairobi Line and Njoro Line.

Tafsiri na Faustine Ngila