HabariSiasa

Matiang'i, Kihalangwa na Boinnet waitwa kortini kuhusu Miguna

March 28th, 2018 1 min read

Na MAUREEN KAKAH

Mahakama Kuu sasa imewaagiza maafisa watatu wa ngazi ya juu serikalini kufika kortini  Jumatano alasiri kuhusu kesi ya uraia wa wakili mbishi Dkt Miguna Miguna.

Jaji George Odunga amewataka Waziri wa Usalama Dkt Fred Matiang’i, Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji Gordon Kihalangwa, na Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet kufika mbele yake saa nane kamili.

 

Habari zaidi kufuata …