Kimataifa

Matokeo ya mwanzo yaonyesha ANC itapoteza viti bungeni, na kulazimika kugawa serikali

May 30th, 2024 1 min read

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

SHUGHULI ya kuhesabu kura ilianza Alhamisi asubuhi huku matokeo ya awali yakionyesha mabadiliko makubwa zaidi ya kisiasa tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi.

Kulingana na takwimu kutoka Tume ya Uchaguzi kutoka kwa asilimia 10 ya vituo vya kupiga kura, mgao wa ANC katika uchaguzi wa Jumatano, ulifikia asilimia 42.3, huku chama kinachounga mkono biashara cha Democratic Alliance (DA) kikipata asilimia 26.3 na chama cha Marxist Economic Freedom Fighters (EFF) kikipata asilimia 8.

ANC huenda kikapoteza wingi wa wabunge, kinyume na miaka 30 iliyopita ambapo kilikuwa kimeshikilia. Ikiwa matokeo ya mwisho yataendelea kuwa kama ilivyojitokeza kwa asilimia kumi, huenda ANC ikalazimika kufanya makubaliano na chama kimoja au zaidi ili kuweza kutawala. Hali hiyo inaweza kusababisha msukosuko wa kisiasa katika wiki au miezi ijayo.

Chini ya katiba ya Afrika Kusini, bunge la kitaifa jipya litamchagua rais mpya.

ANC bado inaaminika kuwa chama kikubwa zaidi chini ya uongozi wa Cyril Ramaphosa, na kuna uwezekano wa yeye kubaki kuwa rais.

Hata hivyo, huenda akakabiliwa na changamoto za uongozi kutoka ndani ya chama.

Matokeo ya mapema yanaonyesha vyama vya ANC na DA kila moja kilipata asilimia 34 katika jimbo muhimu la Gauteng, ambalo linajumuisha mji mkuu wa biashara wa nchi hiyo Johannesburg na vitongoji vilivyoenea vya Soweto na Alexandra.

Kulingana na sheria, Tume ya Uchaguzi ina siku saba kutangaza matokeo hayo, ila huwa inatangaza kabla. Katika uchanguzi wa 2019, upigaji kura ulianza Jumatano na mshindi kutangazwa